- Kasisi wa kanisa Katoliki nchini Tanzania amewataka wanafunzi wenye umri mdogo wanaopachikwa mimba kuchukuliwa hatua kali ya kisheria

- Kasisi huyo alidai kuwa msichana wa shule anayepatikana na ujamzito atakamatwa na maafisa wa polisi na kuzuliwa gerezani bila kujali hali yake

- Kulingana na kasisi huyo ,hiyo ni njia moja ya kupunguza visa vya wasichana wenye umri mdogo kupachikwa mimba kiholela

Kasisi wa kanisa katoliki nchini Tanzania amewashangaza wengi baada ya kudai kuwa wasichana wenye umri mdogo wanaopachikwa mimba watachukuliwa hatua kali ya kisheria.

Leonard Kasimila wa kanisa katoliki la Kitavi alidai kuwa hatua hiyo itakuwa bora kabisa kwa sababu itazuia visa vingi vya wasichana wa shule kupachikwa mimba.

Habari Nyingine: Dadake mhubiri mwenye utata Kanyari aanika utupu wake mitandaoni

Tuma neno ‘NEWS’ kwa 40227 ili kupata habari muhimu pindi zinapochipuka

Hatua hiyo ilizua hisia tofauti miongoni mwa wafuasi wake huku wengine wakidai kuwa ni vyema kutafuta suluhu nyingine kuliko kumkamata mtu akiwa mjamzito.

Habari Nyingine: Picha 14 maridadi za mcheshi Shaniqwa na mpenzi wake

“ Asilimia 80 ya wasichana wenye umri mdogo hupachikwa mimba sana,ili kuliondoa janga hili,wasichana wanaopachikwa mimba pamoja na wazazi wao wanapaswa kukamatwa,” Kasisi huyo alisema.

Haya yanajiri baada ya Rais John Magufuli kutangaza kuwa hatawaruhusu wasichana wa shule kupachikwa mimba na warudishwe shule tena.

Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri: mwangi.muraguri@tuko.co.ke

Tazama habari zaidi kutoka TUKO.co.ke

Subscribe to watch new videos

Chanzo: TUKO.co.ke

ncG1vNJzZmijmajEorTIpaBnrKWgvG%2Bvzmeinmdia4R6hJJmopqrmai2bq3TmqKaZaeWwKqvx5qlmmWnlruiu8%2BamqGhm6yubrnIppmaZaeWuKrDwGaZmpyfYsCpwcuepaJlp5a4ornAra6eZpipuq0%3D