-Kundi la uokoaji la Gavana wa Nairobi Mike Sonko limesusia kazi likilalamikia kutolipwa mishahara
- Timu hiyo ilidai haijalipwa kwa miezi 8 na gavana huyo mashuhuri
- Wafanyakazi hao walifanya maandamano nje ya afisi za City Hall wakidai kukutana na gavana
Wafanykazi wa Sonko Rescue Team shirika lisilo la Kiserikali mnamo Jumanne, Disemba 19, walilalamikia wanachotaja kama kutolipwa malimbikizi ya mishahara kwa muda wa miezi minane iliyopita.
Wafanyakazi hao wenye ghadhabu walipiga kambi nje ya afisi za Gavana Mike Sonko katika City Hall, City Centre na wakadai kukutana na gavana huyo.
Sonko Rescue Team ni NGO iliyosajilishwa na kufadhiliwa na gavana wa kaunti ya Nairobi.
Habari Nyingine: Pata kujua mitaa 8 yenye nyumba zilizo katika hatari ya kubomoka Nairobi
Habari Nyingine: Pata kufahamu zaidi kuhusu maana ya majina haya katika jamii ya Wakikuyu
Wafanyakazi hao, wengi wao wakiwa vijana, walikuwa karibu 120. Walidai kwamba licha ya kutoa huduma, hawajapokea malipo yao katika muda wa miezi 8.
TUKO.co.ke pia ilifahamu kwamba vijana hao sasa wanamwaga taka katika baadhi ya sehemu jijini kama njia ya kulalamikia hatua hiyo.
Tayari, MCA wa Nairobi Magharibi Maurice Gari amelalamikia hatua ya wanachama wa SRT ya kumwaga taka Nairobi West ambayo iko chini ya mamlaka yake.
Habari Nyingine: Mwanafunzi wa kike kutoka Nyeri aliyekamatwa na vifurushi kadha vya bangi katika chupi kulipwa KSh 4 milioni
Gori ametishia kuwaongoza vijana hao katika maandamano afisini mwa gavana ikiwa yeye (Sonko) hatachukua hatua ya dharura.
Hata hivyo, Sonko amepuuzilia mbali vijana hao akisema wanasingizia tu maadamu hawajasajilishwa na NGO hiyo.
Alichapisha picha za vijana wengine wakizoa taka katika eneo la Nairobi West.
Read ENGLISH VERSION
Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe?Tuma ujumbe kwa mhariri:mwangi.muraguri@tuko.co.ke
Subscribe to watch new videosChanzo: TUKO.co.ke
ncG1vNJzZmijmajEorTIpaBnrKWgvG%2Bvzmeinmdia35xgpZmqqimm6R6s7HSnKyeZaSarq551pqnop%2BRYriiucGiZKeilWLGonnAn6CsoV2urm6zwK%2BYp5ldrK6stcuao5qlmaC2onnMopyzoV1te6nAzKU%3D