-Magavana hawataki mtindo wa jadi katika uchaguzi wa Agosti 8, 2017
-Magavana wamependekeza mfumo wa elektroniki ambao wamedai sio rahisi kutumika kuiba kura
Sawia na mrengo wa upinzani wa CORD, magavana wamekataa utumizi wa mfumo wa jadi katika uchaguzi wa Agosti 8 2017.
Habari Nyingine: Wakenya wamshtumu Rais Uhuru Kenyatta kwa unyakuzi wa mashamba
Kulingana na magavana, ni rahisi kutumia mtindo wa jadi kuiba kura ikilinganishwa na ule wa elektroniki.
Magavana Isaac Ruto (Bomet), John Mruttu (Taita-Taveta) na Kivutha Kibwana (Makueni) walipigia debe mfumo wa elektroniki.
Magavana hao waliyasema hayo walipofika mbele ya kamati ya sheria ya seneti iliyopewa jukumu la kutafuta muafaka kati ya pande hizo mbili pinzani.
Pata HAPA habari pindi zinapochipuka
Mrengo wa Jubilee unaunga mkono kutumiwa kwa mfumo wa elektroniki pamoja na ule wa jadi katika uchaguzi huo.
Kwa upande wake Mwanasheria Mkuu Githu Muigai aliunga mkono mfumo utakaoruhusu utumizi wa mfumo wa jadi pamoja na ule wa elektroniki katika uchaguzi huo.
Habari Nyingine: Wahudumu wa matatu wapiga magoti kwa maombi, Nanyuki
Bunge la kitaifa lilipitisha sheria iliyoruhusu utumizi wa sheria ya elektroniki pamoja na ile ya jadi mnamo Disemba 22, 2016.
Kwa mujibu wa wabunge wa Jubilee mabadiliko hayo yataiwezesha Tume ya Uchaguzi nchini, IEBC, kutumia njia ya kawaida kuwatambua wapiga kura na kuwasilisha matokeo ya Urais ikiwa mfumo wa teknolojia hautaweza kufanya kazi yake vizuri.
Hebu tazama video hii ya Mwanasheria Mkuu Githu Muigai akipendekeza mfumo jadi wa uchaguzi:
Subscribe to watch new videosRead ENGLISH VERSION
Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri: aron.mtunji@tuko.co.ke
Chanzo: TUKO.co.ke
ncG1vNJzZmijmajEorTIpaBnrKWgvG%2BvzmeinmdiZ4N1gZNmpJqfkauur62MsJiuppeWeq63zqemZqWimruou4ywmGabn6exbrTAm5iroV2grq61y6JloaydoQ%3D%3D